Mshambuliaji wa pembeni wa Mabingwa wa Hispania Real Madrid, Eden Hazard amesema huenda akarejea jijini London kujiunga na waajiri wake wa zamani Chelsea, kutokana na kukoshwa na aina ya wachezaji wapya ambao wapo njiani kusajiliwa majira ya kiangazi.
Hazard amesema anafikiria kurudi hapo siku moja na mashabiki wa Chelsea wategemee hilo, kwa kuwa mastaa kama Timo Werner na Hakim Ziyech wanampa mzuka wa kutaka kucheza nao.
Chelsea tayari imejihakikishia kuziapata saini za Hakim Ziyech kutoka Juventus na Timo Werner kutoka RB Leipzig, Pia wapo kwenye mpango wa kuhakikisha wanaipata saini ya Kai Havertz wa Bayer Leverkusen ambaye ripoti zinadai wameongeza juhudi za kuhakikisha wanaipata saini yake.
“Nitarudi ikiwa nitamaliza kilichonileta hapa, huwa naangalia mechi zao japo sio mara nyingi, kiukweli wanafanya vizuri, kuna vijana wengi kwenye timu ambao wana viwango vizuri, kwa sasa wanaweza kununua wachezaji kwa bei kubwa kiukweli nafikiri siku moja nitarudi hapo,” alisema.
Hazard anatajwa mmoja kati ya wacheza bora kwenye karne ya 21, huku akiwa ameonyesha kiwango bora katika miaka saba aliyodumu wakati yupo Chelsea akisajiliwa kutoka Lille mwaka 2012.
Fundi huyo mwenye umri wa miaka 29 amefunga jumla ya mabao 110 akiwa na Chelsea na kuiwezesha kuchukua mataji mawili ya Ligi Kuu, taji moja la FA Cup, kombe la ligi na mataji mawili ya Europa League.
Hazard alijiunga na Madrid mwaka jana katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi kwa dau la Pauni 85 milioni na mpaka sasa amefanikiwa kushinda taji moja la Ligi Kuu walilochukua wiki iliyopita baada ya kuwashinda wapinzani wao wa karibu Barcelona ambao walikuwa wanawafukuzia kwenye nafasi ya pili kwa tofauti ya nne.
Hata hivyo, baada ya kufungwa na Osassuna na Madridi kushinda dhidi ya Villarreal tofauti ya alama ikawa ni saba na hatiame Madrid ikanyakuwa taji.