Mama Salma Kikwete, amepata kura za maoni 92 za kugombea nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Katika Jimbo la Mchinga, akifuatiwa na Saidi Mderu, kura 68, watatu ni Liziki Lulida, Kura 62, Abdulazizi Silipi, kura 52.

Fredy Lowassa ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, ameibuka mshindi wa kura za maoni jimbo la Monduli baada ya kupata kura 244.

Mbunge aliyemaliza muda wake Julius Kalanga amepata kura  162, na Wilson Lengima amepata kura 149.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameibuka mshindi wa kura za maoni Jimbo la Tanga Mjini baada ya kupata kura 783 kati ya kura 873 zilizopigwa, Mshindi wa pili ni Omary Ayoub ambaye amepata kura 41.

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameongoza kwa kura 434 kwenye kinyang’anyiro Cha kura za maoni dhidi ya wagombea wenzake tisa. Matokeo hayo ni kati ya kura 597 zilizopigwa.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 22, 2020
Eden Hazard ana ndoto za kurudi Chelsea