Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Rivers United, Stanley Eguma amesema anatambua ubora wa kikosi cha Young Africans kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Rivers United iliyopoteza mchezo wa Mkondo wa Kwanza kwa kufungwa 2-0 nyumbani kwao Nigeria, iliwasili jijini Dar es salaam jana Ijumaa (Aprili 28) majira ya alfajiri ikitokea kwao Nigeria tayari kwa ajili ya mchezo huo, utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kesho Jumapili (Aprili 30).

Kocha Eguma amesema kuwa wamekuja Tanzania kucheza na timu ambayo wanatambua kuwa ni bora na wanaamini kuwa watakutana na upinzani mgumu huku akisema kuwa licha ya yote lakini watahakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Tunafahamu na kuutambua ubora wa wapinzani wetu Young Africans, kwanza tuwapongeze kwa kufanikiwa kupata ushindi ugenini kwa maana ya Nigeria, tumekuja hapa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kama ambavyo wao walifanikiwa.”

“Haina maana kwa kuwa tulifungwa kwetu basi tuje hapa kwa unyonge kwamba tutapoteza mchezo, hapana mpira haupo hivyo. Tutahakikisha kuwa tunaonyesha ubora wetu ili tujiweke katika mazingira mazuri ya kupata matokeo,” amesema Eguma

Ili ifuzu Nusu Fainali Rivers United inapawa kusaka ushindi wa 3-0 ama zaidi dhidi ya Young Africans ambayo inatarajia kucheza mbele na Mashabiki na Wanachama wake, ambao wanatazamiwa kufika kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Young Africans inahitaji sare ya aina yoyote ama ushindi ili kujihakikishia kucheza Nusu Fainali kwa mara ya kwanza katika Michuano hiyo inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Moses Phiri: Nitarudi kwa moto mkubwa
Malisa asisitiza jitihada usimamizi wa usafi jiji la Mbeya