Serikali kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, inaendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa masuala ya maafa nchini, ili kuwa na mikakati thabiti ya kukabiliana na maafa.

Akizungumza wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Anderson Mutatembwa amesema tayari ofisi yake imeendelea kuratibu Mfumo Shirikishi wa kidigitali wa usimamizi wa taarifa za masuala ya maafa.

Ameema, uwepo wa Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, uwepo wa vifaa vya misaada ya kibinadamu vinavyohifadhiwa kwenye maghala, utoaji wa elimu kwa umma pamoja na ujenzi wa kituo cha Usimamizi wa Maafa katika eneo la Nzuguni Dodoma ni moja ya ufanikishaji wa mikakati hiyo.

Kuhusu maandalizi katika kuelekea mvua za El nino, Mutatembwa amesema ofisi imeendela kuziwezesha Kamati za maafa katika mikoa 14 iliyotabiriwa kupata athari za mvua hizo zilizotabiriwa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini na kuzikumbusha kuendelea kujiimarisha katika maeneo yao ili kukabiliana na madhara yanayoweza kutokea wakati wa mvua hizo.

“Tumeshaifikia mikoa iliyotajwa kuathiriwa na mvua za el nino kwa kutoa elimu kwa kamati za maafa ngazi ya Mkoa hadi Vijiji lengo ni kuwajengea uelewa zaidi na kukumbusha jamii kuchukua hatua za mapema kabla ya kupata madhara ya uwepo wa mvua hizo,” alisema Mutatembwa.

Akiwasilisha taarifa kuhusu dhana ya menejimenti ya Maafa na Mfuko wa Taifa wa usimamizi wa maafa nchini, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Charles Msangi ameeleza kuwa, Ofisi hiyo imeendelea kuimarisha mfumo wa mawasilino kupitia kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura kilicho chini ya Ofisi hiyo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Japhet Hasunga ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendelea kuratibu masuala ya maafa nchini huku akiwakumbusha kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu kwa umma na kuwa na mifumo rahisi ya kuyafikia makundi yote nchini kuanzia ngazi ya Kijiji ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya masuala hayo.

Kopunovic ageuka mbogo Tabora United
Temeke yatumia haja kubwa kugundua Kifua Kikuu