Imeelezwa kuwa moja ya changamoto inayowakabili wahitimu wengi wa masomo ya vyuo vikuu nchini ni kukosa ujuzi wa ziada utakaoweza kuwasaidia katika ushindani wa soko la ajira.
Wahitimu wengi wamekuwa wakilalamikia ugumu wa ajira huku pia wengi wao wakiwa hawana ujuzi wa kujiajiri wenyewe licha ya kutumia muda mwingi hadi kumaliza masomo yao ya elimu ya juu.
Afisa uhusiano wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) Doraha Tesha amesema suluhisho la changamoto hiyo itapatikana endapo kila mtanzania atapitia katika mafunzo ya ufundi stafi kwa lengo la kumuongezea ujuzi ili aweze kujiajiri.
Mafunzo yanayotolewa na VETA yanabadilika kuendena na soko la ajira na uhitaji wa changamoto iliyopo kwenye jamii ili kugeuza fursa kwa wahitimu
Asilimia mia ya wahitimu wa VETA wameweza kujiajiri kwa kutumia ujuzi waliojifunza katika vyuo vya ufundi stadi na kuongeza tija ya bidhaa za kibunifu wanazozalisha.