Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Julai 17, 2023 baada ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kampasi ya Pemba, eneo la Mtima Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Aidha , Rais Dk.Mwinyi ameupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kuona umuhimu wa kufungua Kampasi hiyo kisiwani Pemba ikiwa ni sehemu sahihi ya kusogeza huduma za jamii katika sekta ya elimu kwa watu wa Pemba na Watanzania kwa ujumla.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi alieleza kuwa mchango mkubwa wa Chuo hicho kwa taifa na uzoefu waliokuwa nao wa kutoa mafunzo kwa wahitimu walioiva kimaadili, kiuongozi , uadilifu, uzalendo na weledi wa hali ya juu ambazo ni nyezo muhimu kwa mtumishi yoyote anayepewa dhamana ya utumishi wa Umma.

Man Utd yajitafuta usajili wa mshambuliaji
GGML wameonesha njia udhibiti VVU - Dkt. Kikwete