Siku zimepita baada ya kuondoka kwake ila Simba haijampata mtu wa kariba yake, Simba ilicheza vyema upande wa kulia, Emmanuel Arnod Okwi alikuwa imara kuja chini kumsaidia Nicolaus Gyan au Zanna Coulibary alikuwa imara kwenye ratio, alisaidia Simba kufanya hata pressing kuanzia juu.
Siku zimepita hii Simba haina ufanisi kwenye area 14 ‘Golden Square’ sehemu ambayo msimu uliopita walipiga pass nyingi na kupika mabao mengi eneo hilo, ni Okwi pekee alikuwa bora, atachukua Mpira pembeni na kuingia nao mpaka kati, ni kwenye eneo hilo ndipo unauona uwanja wote kwa usahihi, unaweza kutoa pass au kufunga.
Siku zimepita Simba kwenye eneo la mwisho haivutii sana, ipo slow mno wana flow moja tu Mpira pembeni kwa options mbili Mosi ni kudelay kusubiri beki afanye overlapping au cross ila hakuna tena plan tofauti na hapo, Simba inatabirika mno, Okwi alikuwa na flexibility inapokwama A atakuja na B.
Siku zimepita ile triangle imepotea, Okwi pembeni, Haruna kati na Chama pembeni, Simba ilikuwa na ladha tatu tofauti, kwa Haruna Mpira utakaa chini na kumtii, kwa Chama Mpira utakaa chini na mabeki kumtii na kwa Okwi Mpira utakaa chini, mabeki watamtii na nyavu zitamuhidi, Simba is no more like that.
Ujio wa Miquissone ni kujaribu kurejesha Okwi type of football! Jamaa anafaa mno ila atamudu presha za Kariakoo?? Atamudu zile physical battles?? Mtoto flani laini hivi kweli ataviweza viwanja kama Sokoine, Kambarage au Mkwakwani?? Ni kijana mzuri ila anahitaji muda kama aliopewa Okwi.
Itachukua muda Simba kutulia hata Real Madrid iliyumba baada ya Ronaldo kuondoka, kwenye hii dunia kuna wachezaji ni kazi kuwapata na kazi kuziba pengo lao.