Mlinda mlango wa klabu ya Young Africans Metacha Mnata ambaye kwa sasa amejihakikishia kuwa kipa namba moja wa kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria, amesema ana ndoto za kucheza soka nje ya nchi.

Metacha amesema lengo la kila mchezaji ni kupata maendeleo katika masha yake ya soka, hivyo hata yeye ana ndoto za kusonge mbale na kuwa sehemu ya wachezaji watanzania wanaocheza soka nje ya nchi.

Mlinda mlango huyo aliyekua kikwazo kwa Simba SC kuzisalimia nyavu za Young Africans kwenye mchezo wa Machi 08 uliomazika kwa mabingwa watetezi kufungwa bao moja kwa sifuri, ameweka wazi mpango huo katika kipindi hiki ambacho anafanya mazoezi binafsi, kufuatia kambi za timu kuvunjwa ili kupisha sakata la maambukizi ya virusi Vya Corona.

“Suala la kwenda kucheza soka nje ya nchi huwa nalifikiria. Nadhani ni ndoto ya kila mchezaji, naendelea kujituma na kufanya mazoezi kwa bidii ili siku moja niweze kufanikiwa,”

Metacha alitua Young Africans mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mbao FC ambao walimsajili kwa mkopo kutoka kwa mabingwa wa kombe la shirikisho (ASFC) Azam FC.

Msimu wake wa kwanza na Young Africans umekuwa mzuri na hata kuweza kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza mbele ya Mkenya Farouk Shikhalo ambaye walisajiliwa kwa lengo la kuwa chaguo la kwanza.

Makali ya Metacha yalianza kuonekana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu wa 2019/20, akipata nafasi ya kukaa langoni kwenye michuano hiyo kufuatia kibali cha Shikhalo kuchelewa.

Alitoa mchango mkubwa kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ugenini kule Botswana, ambako Young Africans walifanikiwa kushinda bao moja kwa sifuri dhidi ya Township Rollers, Katika mchezo huo Metacha aliokoa mkwaju wa penati.

Corona Tanzania: Vifo viwili vyaongezeka, wagonjwa wapya 7
Emmanuel Arnod Okwi - Kete inayokosekana kwenye draft la Simba SC