Wizara ya Afya imetangaza vifo vya wagonjwa wawili wa Covid 19 vilivyotokea leo Aprili 10, 2020 na kufanya idadi ya waliofariki kwa ugonjwa huo hapa nchini kufikia watatu.

Taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa waliofariki Wote ni wanaume raia wa Tanzania kutokea jijini Dar es Salaam. Mmoja akiwa na umri wa miaka 51 na mwingine akiwa na miaka 57.

Halikadharika wizara pia imetangaza waathirika wapya watano; wanaume wanne na Mwanamke mmoja. Wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Mapema leo waziri wa afya, Zanzibar alitangaza kuongezeka kwa wagonjwa wawili , hivyo kwa sasa Tanzania bara na visiwani kuna waathirika wa virusi vya Coroana 32.

Visa vya maambukizi ya virusi vya corona kote duniani vimepindukia milioni 1.5 leo huku idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 imepanda hadi watu 89,400.

Sababu yatajwa Tanzania kutowekwa karantini
Ndoto za Metacha Mnata sio Young Africans