Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid ametangaza kupatikana kwa wagonjwa wawili raia wa Tanzania wenye maambukizi ya virusi vya Corona na kufanya idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo visiwani humo kufikia 9 mpaka sasa.

Waziri Hamd amesema raia hao wa Tanzania waliopatikana na virusi hivyo hawakuwahi kusafiri nje ya visiwa vya Zanzibar tokea mlipuko wa corona uanze mwishoni mwa mwaka 2019.

Jana waziri wa afya nchini Tanzania, Ummy mwalimu alitangaza kuwa maambukizi ya ndani ya nchi yameanza hivyo jitihada zaidi za kupambana na ugonjwa huo zinahitajika.

Yondani ampigia chapuo Mwamunyeto
CORONA: Southampton kukatwa mshahara