Ukarimu wa mpachikaji mabao wa Manchester City, Erling Haaland umemkasirisha Meneja wa Klabu hiyo Pep Guardiola baada ya mshambuliaji huyo kutoka Norway kupuuza maagizo ya kumtaka kupiga mkwaju wa Penati na kuamuachia Ilkay Gundogon.
Baada ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani kufunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuwatanguliza vinara hao wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Leeds United, Guardiola alikuwa akipiga kelele toka nje ya uwanja ya kutaka Haaland kupiga mkwaju wa Penati waliyopata dakika za mwisho za mchezo huo.
Lakini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 na ambaye tayari ameweka rekodi ya kufunga mabao mengi ya Ligi Kuu ya England kwa msimu mmoja ya mabao 35, alimtazama Guardiola na kuamua kumpa Gundogon kupiga mkwaju wa Penati ili kukamilisha idadi ya mabao matatu.
Ni uamuzi ulioonekana kumchukiza Guardiola hasa baada ya penalti hiyo ya Gundogon kuokolewa na kipa Joel Robles.
“Lakini mpigaji Penati ni mpigaji Penati. Lakini tukiwa mbele kwa mabao 2-0 hii ni kazi, sio suala kwamba hauwezi kuja kusahau”
Gundogon mwenye umri wa miaka 32 alihisi hasira za Guardiola wakati akienda kupiga mkwaju ule wa Penati.
“Kwanza alimuonyesha Erling kwamba anashauku ya kupiga mkwaju ule wa Penati lakini pia alinikasirikia mimi,” alisema Gundogan alipozungumza na BBC Sport. “Hivyo ndivyo ilivyokuwa mwishoni.
“Wakati Erling amechukua ule mpira, nilikuwa na uhakika anaenda kupiga mkwaju ule wa Penati. Nilimungalia mara kadhaa kuona kuwa alikuwa na uhakika na alidhamiria.”