Shirikisho la soka barani Afrika CAF, imetangaza majina 30 ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa bara hilo kwa mwaka 2017, huku likimtema mshindi wa mwaka jana Riyad Mahrez.
Mahrez, ameachwa kwenye orodha hiyo kutokana na kutokua na kiwango kizuri cha soka kwa mwaka huu, kama ilivyokua msimu wa 2015/16, ambapo alichangia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha klabu yake ya Leicester City kutwaa ubingwa pamoja na kuiwezesha Algeria kufuzu fainali za Afrika za mwaka huu zilizofanyika nchini Gabon.
Katika orodha hiyo mshindi wa mwaka 2015, nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Gabon’s Pierre-Emerick Aubameyang, amejumuishwa sambamba na wachezjai wengine wa Afrika wanaosukuma soka huko barani Ulaya kama Sadio Mane wa Senegal ambaye alishika nafasi ya tatu mwaka 2016.
CAF pia amemjumuisha mlinda mlango wa kikosi cha timu ya taifa ya Misri Essam El Hadary mwenye umri wa miaka 44, ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa kuipeleka nchi yake kwenye fainali za kombe la dunia za 2018.
Mlinda mlango huyo, kwa sasa anacheza soka nchini Saudi Arabia kwenye klabu ya Al-Taawoun.
Orodha hiyo ya wachezaji 30 iliyotolewa hii leo na CAF, ni wachezaji wanne pekee ndio wanacheza soka ndani ya Afrika, na wengine 26 wanacheza nje ya bara hilo.
Wachezaji hao ni Ali Maaloul wa Tunisia na klabu ya Al Ahly ya Misri, Percy Tau wa Afrika kusini na mlinda mlango kutoka nchini Uganda Dennis Onyango (wote wanacheza Mamelodi Sundowns) na Fackson Kapumbu wa Zambia na klabu ya Zesco United.
Shughuli ya kumtangaza mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2017, imepangwa kufanyika mjini Accra nchini Ghana, Januari 04 mwaka 2018.
Makocha wa timu za taifa na wakurugenzi wa ufundi wa mataifa wanachama wa CAF watahusika katika kupiga kura za kumchagua mchezaji bora.
Orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya Afrika mwaka 2017.
Vincent Aboubakar (Cameroon & FC Porto), Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord), Christian Atsu (Ghana & Newcastle), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund), Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester United), Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal), Keita Balde (Senegal & Monaco), Christian Bassogog (Cameroon & Henan Jianye), Yves Bissouma (Mali & Lille) na Khalid Boutaib (Morocco & Yeni Malatyaspor).
Wengine ni Yacine Brahimi (Algeria & Porto), Essam El Hadary (Egypt & Al Taawoun), Junior Kabananga (DR Congo & Astana), Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco), Naby Keita (Guinea & RB Leipzig), Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly), Sadio Mane (Senegal & Liverpool), Moussa Marega (Mali & Porto), Victor Moses (Nigeria & Chelsea), Youssef Msakni (Tunisia & Al Duhail), Michael Olunga (Kenya & Girona) na Fabrice Ondoa (Cameroon & Sevilla)
Pia yupo Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns), Thomas Partey (Ghana & Atletico Madrid), Mohamed Salah (Egypt & Liverpool), Mbwana Samata (Tanzania & Genk), Jean Michel Seri (Cote d’Ivoire & Nice), Percy Tau (South Africa & Mamelodi Sundowns), Bertrand Traore (Burkina Faso & Lyon) na William Troost-Ekong (Nigeria & Bursaspor).
Orodha ya wachezaji wanaowani tuzo ya mchezaji bora wa ndani ya Afrika (African Player of the Year – Based in Africa).
Nasr Eldin Ahmed (Sudan & Hilal Obeid), Junior Ajayi (Nigeria & Al Ahly), Karim Aouadhi (Tunisia & CS Sfaxien), Aristide Bance (Burkina Faso & Al Masry), Alkhaly Bangoura (Guinea & Etoile du Sahel), Achraf Bencharki (Morocco & Wydad Athletic Club), Jeremy Brockie (New Zealand & Supersport), Fawzi Chaouchi (Algeria & MC Alger), Oussama Darfalou (Algeria & USM Alger), Muaid Ellafi (Libya & Ahly Tripoli), Tady Etekiama (DR Congo & AS Vita) na Ahmed Fathi (Egypt & Al Ahly).
Wengine ni Dean Furman (South Africa & Supersport United), Sylvain Gbohouo (Cote d’Ivoire & TP Mazembe), Tarek Hamed (Egypt & Zamalek), Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco), Saber Khalifa (Tunisia & Club Africain), Taha Yassine Khenissi (Tunisia & Esperance), Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly), Ayman Majid (Morocco & FUS Rabat), Ben Malango (DR Congo & TP Mazembe) na Aymen Mathlouthi (Tunisia & Etoile du Sahel).
Pia yupo Mohamed Meftah (Algeria & USM Alger), Sabelo Ndzinisa (Swaziland & Mbabane Swallows), Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns), Mohamed Ounnajem (Morocco & Wydad Athletic Club), Elsamani Saadeldin (Sudan & Al Merreikh), Saladin Said (Ethiopia & Saint George), Geoffrey Serunkuma (Uganda & KCCA), Percy Tau (South Africa & Mamelodi Sundowns).