Umoja wa Ulaya (EU) umeituhumu Urusi kwa Uhalifu wa kivita nchini Ukraine. Kwa mujibu wa azimio la viongozi wa umoja huo Urusi itaadhibiwa kwa sheria za kimataifa.
Umoja huo umesema baada ya mkutano wao wa kilele wa mjini Brusseles, serikali ya Urusi itawajibishwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Azimio la Baraza la Umoja wa Ulaya linasema Urusi imekuwa ikiratibu mashambulizi dhidi ya umma wa watu na kuyalenga maeneo ya umma, vikiwemo hospitali, viwanda vya madawa, shule na makazi. Na kumalizia huo ni uhalifu wa kivita lazima usitishwe mara moja.
Na kundi la mataifa yenye nguvu ya kiwanda duniani yaani G7 yameonya dhidi ya kutumika kwa silaha yoyote ya maangamizi dhidi ya Ukraine, kwa kusema Urusi inadhibitiwa na mikataba ya kimataifa.
Baada ya mkutano wao wa kilele wa dharura kuhusu uvamizi wa Ukraine, taarifa ya pamoja ya mataifa hayo ilitoa onyo la kutumika kwa silaha za kikemikali, bailojoia, nyuklia au zozote zenye kufanana na hizo. Imeitaka Urusi kutimiza matakwa ya makubaliano ya kimataifa,ambayo Urusi imesaini ya kulinda kila mmoja.