Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania David Concar amesema kuwa wanaridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu.

Ameyasema hayo hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 21,2022 kabla ya kuanza ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Uingereza.

Amesema kuwa Rais Samia amekuwa akifanya teuzi mbalimbali za uongozi kwa usawa ambapo hali hiyo imesaidia masuala ya kisiasa kuzidi kuboreshwa zaidi.

Amesema mahusiano mazuri anayoyajenga Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu na Nchi mbalimbali ni mahusiano yenye tija kwa uchumi imara wa Taifa na mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza ( MPC), Edwini Soko amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania vyombo mbalimbali vya habari vimeimerika kwa kuwa na uhuru wa kuripoti maudhui mbalimbali yenye tija kwa Jamii

Ujenzi wa mzani kemondo wapandisha mapato
Polisi watakiwa kuusoma ulimwengu wa mitandao