Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kushuka kwa bei ya Petroli na Dizeli kwa asilimia 2.7 (shilingi 61) na asilimia 3.8 (Shilingi 88) na ongezeko la asilimia 0.09 (shilingi 2) kwa mafuta ya taa.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Mamlaka hiyo na kusisitiza kuwa bei hizo zitaanza kutumika rasmi leo Mei 02, 2018 kwa nchi nzima.
EWURA imesema kubadilika kwa bei hizo kumetokana na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia na kupungua kwa gharama za usafirishaji wa mafuta (BPS Premium) pamoja na kuchangiwa kwa kubadilika kwa kanuni ya kukokotoa bei za mafuta nchini ili kujumuisha gharama kwa wakala wa serikali na tozo za huduma za Manispaa na Jiji kwa wauzaji wa mafuta kwa jumla na rejareja.
“Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani,”imesema taarifa
Hata hivyo, kwa upande mwingine EWURA imewataka wauzaji wa mafuta ya petroli kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) huku wanunuzi wakiombwa kuhakisha wanapata stakabadhi.
-
Ajiua kisa wivu wa mapenzi
-
Waziri ampigia magoti JPM, asema yaliyopita si ndwele
-
Heche: Tutapokea msaada kwa mtu yeyote lakini siyo polisi