Mkazi mmoja wa Katoro-Geita aitwaye, Maganiko Nunda amejiua kwa kunywa sumu baada ya kutokea kwa mgogoro na mke wake siku nne zilizopita.

Inadaiwa kuwa mgogoro huo unahusu unywaji wa pombe kupindukia uliosababisha mkewe kumkimbia siku nne zilizopita.

Mtoto wa marehemu ndiye aliyesimulia kilichotokea baada ya kwenda kumsalimia baba yake huyo na kukuta amefariki huku akitokwa na povu mdomoni na puani.

Aidha, kabla ya kuchukua uamuzi huo wa kujiua marehemu ameacha ujumbe kwenye barua usemao kuwa “kwakuwa nimekuwa kero kwa familia yangu nimeamua kujiua”

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Geita amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ila hajasema ni sumu gani marehemu alitumia.

 

Alikiba rasmi atangaza ujio wa kinywaji chake ''Mofaya''
Iran yazikana nyaraka za Israel, yasema ni za uchochezi