Msanii wa Muzuki wa kizazi kipya nchini anayefanya vizuri kwenye tasnia hiyo, Ali Kiba ameitambulisha rasmi bidhaa yake kinywaji kinachoenda kwa jina la Mofaya Energy Drink akiwa ameshirikiana na msanii mwenzake Djbulive bidhaa ambayo inatarajia kufanya vizuri ndani na nje ya Afrika.

Alikiba kwa mara ya kwanza aliitambulisha bidhaa hiyo katika harusi yake iliyofanyika jumapili ya tarehe 29.4.2018 katika ukumbi wa Serena hoteli.

Mapema leo hii ametumia ukurasa wake wa intagram kuandika.

”Kwa heshima kubwa nina furaha kuwatangazia ujio wa bidhaa yangu ya kwanza Mofaya Energy Drink. Kwa kushirikiana na msanii mwenzangu @djbuliv tutawaletea bidhaa East Afrika na Afrika nzima na Mungu akijalia tutaifikisha duniani kote. Bidhaa ni yetu waafrika na inatengenezwa ndani ya Afrika. Ni zamu ya kwetu Afrika kutengeneza bidhaa zetu na kuzifikisha ulimwenguni kote na pia kupatia fursa vijana wenzetu.

Katika andiko hilo Alikiba amemalizia kwa kuandika ”Huu ni muda wetu sasa waafrika kuwa wajasiliamali”.

Aidha Alikiba ni moja ya wasanii wakongwe katika tasnia ya muziki wa bongo fleva jitihada zake, uwezo wake umekuwa ukionekana kupitia kazi mbalimbali anazozifanya, kama msanii mkubwa nchini, hii ni moja ya hatua kubwa ambayo kama kioo cha jamii ni mfano wa kuigwa kutokana na mchango mkubwa unaoutoa kupitia kuanzishwa kwa bidhaa hiyo.

 

Marekani yaituhumu Iran kuvuruga amani ya Mashariki ya Kati
Ajiua kisa wivu wa mapenzi