Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo ameituhumu Iran kwa shughuli zake katika ukanda wa Mashariki ya Kati, ambazo amesema kuwa zinauvurga ukanda huo.

Ameyasema hayo wakati Waziri Mkuu wa Israel,  Benjamini Netanyahu akisisitiza kuwa makubaliano ya nyukilia na Iran lazima yabadilishwe au yavunjwe ingawa mataifa mengine yanaunga mkono makubaliano hayo.

Mike Pompeo  amesema kuwa nia ya Iran kutaka kutawala siasa za  Mashariki ya Kati bado ipo palepale na akasema hawatapuuza vitendo hivyo vya Iran kama ilivyokuwa kwa utawala uliotangulia.

Aidha, amesisitiza kuwa rais Donald Trump atajiondoa kwenye makubaliano ya nyukilia na Iran iwapo hayatafanyiwa mabadiliko huku waziri mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu akiongeza kuwa kiu ya Iran kutaka kutengeneza bomu la nyukilia lazima izuiwe ikiwa ni pamoja na uchokozi wake.

Hata hivyo, kwa upande wake rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kuwa makubaliano ya nyuklia na Iran hayawezi kujadiliwa upya.

 

 

Waziri ampigia magoti JPM, asema yaliyopita si ndwele
Alikiba rasmi atangaza ujio wa kinywaji chake ''Mofaya''