#PenyenyeZaKitaa ni kipindi kinacholenga kuburudisha zaidi na kuelimisha. Maswali yote yanayoulizwa yanaulizwa ki-Penyenye na majibu yanatolewa ki-Penyenye na ndipo lengo kuu la kuburudisha zaidi linaonekana huku elimu pia ikichukua mkondo wake.
Kipindi kilianza na msimu wa kwanza kikafanya vyema na sasa ni msimu wa pili ambapo swali linasema hivi: Ukimkuta Mume/mke wako ana ‘KISIMBUSI’ utafanyaje. ??
Kumbuka KISIMBUSI ni King’amuzi (Decoder’) na mfano wa Kisimbusi ni Azam, Star Times na DSTV na vingine vingi.
Ukibofya hapa chini unapata uwezo wa kujikuta upo mtaani ukishuhudia wana Morogoro waki-Penyenye-ka na neno Kisimbusi #Elimika #Burudika #Vunja mbavu………
NB: Wanaojibu maswali ya #PenyenyeZaKitaa wakakosea si kwamba hawana akili ila maswali yanaulizwa kwa aina ya chemshabongo ambayo mtu yeyote anaweza kupatia au kukosea hata wewe pia unayetazama hapa.