Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City wamepangwa kukutana na Chelsea katika Mzunguuko wa Tatu wa Michuano ya Kombe la FA, itakayoendelea mwezi Januari 2023.
Mpambano huo unatarajiwa kuwa na vuta ni kuvute kutokana na ubora wa timu zote mbili, huku kila upande ukihitaji kufanya vyema kwenye mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.
Upinzani wa pande hizo mbili unachagizwa na matokeo ya hivi karibuni, zilipokutana kwenye mchezo wa Kombe la Ligi ‘Carabao Cup’ ambapo Chelsea ilitupwa nje kwa kufungwa 2-0.
Hata hivyo Manchester City watakua nyumbani Ettihad Stadium, kama ilivyokua katika mchezo wa mwisho walipokutana na Chelsea.
Katika hatua nyingine Mabingwa watetezi wa Michuano hiyo Liverpool wamepangwa kuikabili Wolverhampton Wanderers nyumbani katika Uwanja wa Anfield, huku Mashetani Wekundu ‘Manchester United’ watakuwa nyumbani ‘Old Trafford’ kuikabili Everton.
Vinara wa Ligi Kuu ya England kwa sasa Arsenal, ambao wameshatwaa Ubingwa wa Kombe la FA mara 14, watalazimika kusafari kuifuata Oxford United inayoshika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Daraja la pili.
Mzunguuko wa Tatu wa Kombe la FA umepangwa kuchezwa kati ya Januari 6 hadi 9, 2023.
Michezo mingine ya Mzunguuko wa tatu wa Kombe la FA.
Preston v Huddersfield
Middlesbrough v Brighton
Chesterfield v West Brom
Charlton or Stockport County v Walsall
Boreham Wood v Accrington
Tottenham v Portsmouth
Derby v Barnsley
Cardiff v Leeds
Brentford v West Ham
Bournemouth v Burnley
Coventry v Wrexham
Norwich v Blackburn
Aston Villa v Stevenage
Luton v Wigan
Fleetwood v QPR
Grimsby v Burton
Blackpool v Nottingham Forest
Dagenham & Redbridge or Gillingham v Leicester
Forest Green v Birmingham
Bristol City v Swansea
Hartlepool v Stoke
Hull v Fulham
Crystal Palace v Southampton
Millwall v Sheffield United
Shrewsbury v Sunderland
Sheffield Wednesday v Newcastle
Reading v Watford
Ipswich v Rotherham