Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk ameshtakiwa na Chama cha Soka England ‘FA’ kwa kosa la utovu wa nidhamu ikidaiwa alimtolea lugha chafu mwamuzi wa kati baada ya kadi nyekundu katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle, mwishoni mwa juma lililopita.

Nahodha huyo wa Liverpool alitolewa nje baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Newcastle, Alexander Isak wakati anajaribu kufunga bao kwenye Uwanja wa St James Park. Liverpool ilishinda mabao 2-1.

Gazeti la Mail Sport limeripoti Van Dijk anaweza kukosa mechi kwa kufungiwa baada ya kumpinga mwamuzi na alionekana akibishana na mwamuzi wa akiba Craig Pawson baaada ya mchezo huo kumalizika.

Taarifa ya FA iliyotolewa juzi Jumanne ilisomeka: “Inadaiwa beki huyo alicheza rafu na alitumia maneno ya matusi kwa mwamuzi aliyechezesha mchezo baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 29.

“Virgil Van Dijk amnepewa muda wa wa kujitetea hadi kesho Ijumaa kabla ya kuwasilisha majibu kutokana na tukio hilo.

Hadi tukio linatokea beki huyo na wawakilishi wake hawajatoa tamko kama wamekubali au kukana mshataka hayo.”

Kulingana na miongozo ya FA mwenendo huo umetajwa kuwa ni utovu wa nidhamu na utashughulikiwa na kamati husika. Na endapo beki huyo atashindwa kujitetea na kuhukumiwa anaweza kulimwa faini.

Mwaka 2015, alishuhudiwa mchezaji wa zamani wa Arsenal, Gabriel Paulista akifungiwa mechi moja baada kumpinga mwamuzi wa kati alipotolewa kwa kadi nyekundu.

Kwa upande wa Van Dijk alitakiwa kukosa mechi tatu kufuatia kadi nyekundu, lakini kwa tamko la FA huenda adhabu yake ikaongezeka.

Beki huyo alilimwa kadi nyekundu mwishoni mwa juma lililopita kwa mara ya kwanza tangu alipotua klabuni hapo kwa rekodi ya usajili wa Pauni 75 milioni.

Utumishi wahimizwa ushirikiano kuongeza ufanisi wa kazi
Onana awatuliza mashabiki, wachambuzi