Mkuu wa kitengo cha michezo katika kampuni ya Facebook Deen Reed amesema kuna uwezekano wa kampuni hiyo kuwasilisha ombi la kutaka kununua haki za kuonyesha moja kwa moja mechi za ligi ya Uingereza huku uvumi kuhusu hatua hiyo ukitanda.

Kwa sasa BT sport na SkySport ndizo kampuni zenye haki za kuonyesha mechi hizo lakini haki za kuonyesha mechi za ligi hiyo zinatarajiwa kupigwa mnada mwaka ujao.

Akiwa mjini London Deen Reed ambaye ni mkuu wa kitengo cha michezo wa Facebook baada ya kuulizwa kama angewasilisha ombi la kununua hali za ligi hiyo alisema ligi ya Uingereza ni washirika muhimu sana kwao na upo uzekano wa kufanya nao kazi kwa karibu.

 

Facebook umekuwa mtandao maarufu dunia na ulipokea zaidi ya dola bilioni 20 mwaka uliopita mapato mengi yakitoka katika matangazo ya mitandaoni baada ya kuzinduliwa mwaka 2004.

Kampuni hiyo ina takribani wateja bilioni 2 kila mwezi na milioni 650 kati yao ni mashabiki wa michezo huku wengine milioni 200 wakiwa katika mtandao wa picha wa Instagram.

 

 

 

 

 

 

 

Video: Familia ya Lissu yatoa msimamo wake
Majaliwa awapa neno wanafunzi wa kike nchini