Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Fadhili Majiha ‘Stopper’ anatarajia kurejea ulingoni Juni 30, mwaka huu katika pambano ambalo Mfaume Mfaume atacheza na Nkululeko Mhlongo raia wa Afrika Kusini.

Pambano hilo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Promosheni ya PAF Promotion Entertainment Company LTD linatarajia kufanyika Juni 30, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Fadhili Maogola amesema kuwa tayari washamalizana Majiha kwa ajili ya kucheza pambano hilo ambapo kwa sasa wanajipanga kumalizana na mpinzani wake ambaye bado hajawekwa wazi.

“Baada ya Mfaume Mfaume ‘Mapafu ya Mbwa’ sasa tumemalizana na Fadhili Majiha ‘Stopper’ kuelekea kwenye pambano letu la hata usipolala pata kucha kwa sababu hakuna ambaye hajui ubora naukubwa wa Majiha akiwa ni bondia anayekamata nafasi ya pili katika mabondia bora Watanzania kwa sasa.”

“Kilichobakia kwa sasa ni kwamba tunaweka mipango na mikakati yetu vizuri na kuweza kumalizana na mpinzani wake, hatuwezi kumtaja kwa sababu mambo ya kibiashara hadi pale tutakapokuwa tumemalizana naye kwa maana ya kusaini mkataba kwa ajili ya pambano letu,” amesema Maogola

Diarra ajivunia rekodi Ligi Kuu Tanzania Bara
Ulafi wamuingiza Paka kwenye rekodi za Dunia