Michirizi na utomvu unaopatikana katika Bamia, husaidia kusawazisha Kisukari kwa kuzuia kiwango cha Sukari inayotumika katika mwili kutoka kwenye utumbo mkubwa.
Utelezi wa bamia huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali na asidi ya Nyongo unaoingia kutoka kwenye Ini ambao usipo dhibitiwa huenda ikasababisha matatizo ya ki-afya.
Bamia husaidia kulainisha Utumbo mkubwa kutokana na kazi yake ya kulainisha choo lakini pia hutumika kwa kutibu vidonda vya Tumbo inasaidia kusawazisha Asidi.
Bamia ina Vitamin C ambayo inawafana watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe ya Bamia iliyopikwa huwa na miligramu 13 ya vitamin C.
Unashauriwa kutumia nusu kikombe cha Bamia iliyopikwa inakua na kiwango cha 460 IU ya vitamin A. ambayo inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa wa mtoto wa jicho.