Fainali ya mashindano ya vilabu bingwa barani Ulaya iliyochezwa jana kati ya Real Madrid na Juventus imesababisha kujeruhiwa kwa mashabiki 1000 nchini Italy mara baada ya kuzuka kwa taarifa za magaidi kushambulia eneo la Piazza San Carlo walipokuwa wamekusanyika kwaajili ya kutizama mechi hiyo.
Dakika chache mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo kulizuka taarifa za magaidi kushambulia eneo hilo kutokana na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamejitokeza kufuatilia mchezo huo ambao ulivuta hisia za wengi huku Real Madrid wakiibuka na ushindi mnono wa goli 4-1.
Hata hivyo, kitendo hicho cha mashabiki hao kusukumana kwa hofu ya magaidi kushambulia eneo hilo, kilikumbusha tukio la mwaka 1985 katika uwanja wa Heysel ambapo waliuawa mashabiki wa Juventus 39 kwa kudondokewa na ukuta.