Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii wametoa elimu kwa Familia zaidi ya 760 juu ya kutumia Dawa ya kutibu Maji, ili kuzuia Magonjwa ya mlipuko wajati huu wa kipindi hiki cha maafa katika mji mdogo wa Katesh uliopo Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kufanya kikao cha kuwashukuru Wadau pamoja ambao wamekuwa bega Kwa bega na Serikali katika utoaji wa huduma na misaada kwa Waathirika wa Mvua ya Mafuriko.
Amesema, “tumeleta Dawa za kutibu maji, katika kuhakikisha tunaimarisha suala la Kinga dhidi ya Magonjwa ya mlipuko tayari Wahudumu wa Afya wamefikia familia 760 kutoa elimu namna ya Matumizi ya dawa ya kutibu maji na hii itasaidia kwenye suala la kuzuia Magonjwa yatokanayo na maji. ”
Hata hivyo, Dkt. Mollel amesema asilimia 98 ya Majeruhi ambao ilitakiwa wakatiwe rufaa wametibiwa ndani ya Mkoa wa Manyara, kutokana na Serikali kujipanga na kuimarisha huduma za kibingwa.