Ili kufanikiwa na kuwa mtu unayetaka kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo mara nyingi mtu anakuwa anafanya bila kujua matokeo yake leo nakuchorea mambo makuu matano ambayo unatakiwa kuachana nayo ili kuwa mtu unayetaka kuwa.
Usiwe mwenye malengo madogo, ili ufanikiwe inatakiwa kuwa mtu mwenye malengo makubwa, wengi waliofanikiwa katika maisha ni wale ambao walikuwa na malengo makubwa katika maisha, kuwa na malengo makubwa inakufanya kila siku ufanye kitu kufikia lengo lako, malengo madogo huyadumu, na mara nyingi mtu mwenye malengo madogo hufikiria kuwa tajiri ndani ya muda mfupi, wahenga wanasema hata mbuyu ulianza kama mchicha.
Acha kufanya kitu kwa udogo, kila siku fikiria kufanya kitu kikubwa, kwenye biashara yako, kazi yako, kipaji chako usijichukulie kama mtu mdogo, fanya kitu kikubwa kionekane na watu usijishushe na kujiona huwezi muda wote fikiria wewe unaweza kufanya jambo kubwa ongeza thamani katika kila kitu unachokifanya, kuna wakati tunakata tamaa lakini tusiache kujituma kwa kile kitu tunachokiamini na tuwekeze jitihada zetu.
Usiwe mtu wa kutoa sababu katika kila kitu, wazungu wanasema ”excuses make faluire” ukiwa mtu wa sababu sana utashindwa kufanya jambo la maana utakuwa kila kitu unakitafutia sababu, kuliko kutofanya kabisa inashauriwa kufanya halafu ukafeli utajifunza kitu kikubwa ambacho kitaongeza thamani katika kazi yako.
Kubali na amini kuwa sio kila kitu utachofanya kitamfurahisha mtu na usifanye kitu kwa ajili ya kumfurahisha mtu, watu wengi wanafeli hapo wanaangalia nafsi za watu wengine na kuziridhisha na kujisahau wao wenyewe kuwa ndio madereva wa maisha yao, sio kila mtu atafurahia mafanikio yako, wapo watakao kukatisha tamaa katika kila jambo utakalofanya.
Achana na watu ambao ni sumu katika maisha yako, angalia watu wanaokuzunguka, tumia muda wako na watu ambao wanakitu kikubwa kukuzidi wewe utajifunza kitu kutoka kwao, ukiwa umezungukwa na marafiki walevi lazima uwe mlevi, ukitumia muda wako na wachawi lazima uwe mchawi tu, ukitumia muda wako na wajasilimia mali lazima utajifunza ujasilia mali.
Hizo ndizo kanuni na nguzo kuu katika maisha yenye mafanikio, lazima tuishi na kujifunza kitu kipya kila iitwapo leo.