Uchaguzi wa marudio nchini Kenya huenda ukaahirishwa kufanyika tarehe 17 mwezi ujao na kusogezwa mbele kwaajili ya kutatua kasoro mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza ili kuweza kuondokana na matatizo ambayo yanaweza kutokea.

Hayo yametokana na Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, kukutana na kuangalia uwezekano wa kuahirisha Uchaguzi huo baada ya Kampuni moja ya Ufaransa ya Safran Morpho kuomba muda zaidi kuboresha mitambo inayotumiwa kuwatambua wapiga kura.

Aidha, mbali na hilo, Muungano wa Vyama vya Upinzani NASA, unaoongozwa na Raila Odinga, umesema Uchaguzi hautafanyika iwapo marekebisho hayatafanyika ndani ya Tume ya Uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujiuzuru kwa Ezra Chiloba Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.

Hata hivyo, Chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais, Uhuru Kenyatta kimesisitiza kuwa uchaguzi huo ufanyike kama ulivyopangwa.

Fanya hivi kuwa mtu unayetaka kuwa
Rais Dkt. Shein aanza kupanga mikakati ya ushindi 2020