Mashabiki wa klabu za Barcelona na Atletico Madrid wamelishutumu shirikisho la soka duniani FIFA, baada ya kutangaza orodha ya mwisho ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa shirikisho hilo.
Luka Modric, Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah wametajwa kuwania tuzo hiyo ya FIFA jana jumatatu, huku majina ya Lionel Messi na Antoine Griezmann yakiondolewa.
Mashabiki wa klabu hizo za Hispania wameonyesha hasira zao kupitia mitandao ya kijamii, ambapo wameeleza kuchukizwa na hatua hiyo kutokana na kuamini kuwa, wachezaji hao walipaswa kuwa miongoni mwa wanaostahili kuwania tuzo kwa mwaka huu 2018.
Mshabiki hao wameeleza kuwa, wachezaji hao wamekua katika kiwango cha hali ya juu msimu uliopita na wamezisaidia timu zao kufanya vyema katika ligi ya Hispania pamoja na michuano mingine, tofauti na Luka Modric, Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah ambao watawania wapo kwenye orodha ya mwisho.
Mbali na orodha hiyo ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA kwa mwaka 2018, shirikisho hilo limetangaza orodha nyingine za watakaowania tuzo mbalimbali.
Tuzo Ya Kipa Bora
Thibaut Courtois (Real Madrid, Ubelgiji), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur, Ufaransa) na Kasper Schmeichel (Leicester City, Denmark).
Tuzo Ya Kocha Bora Wa Kiume.
Zlatko Dalić (Croatia), Didier Deschamps (Ufaransa) na Zinedine Zidane (Real Madrid).
Mchezaji Bora Wa Kike.
Ada Hegerberg (Lyon, Norway), Dzsenifer Marozsán (Lyon, Ujerumani) na Marta (United States Orlando Pride, Brazil).
Tuzo Ya Kocha Bora Wa Kike.
Reynald Pedros (Lyon), Asako Takakura (Japan) na Sarina Wiegman (Uholanzi).
Tuzo Ya Goli Bora.
Mchezaji | Mchezo | Mashindano | Tarehe | ||
Gareth Bale | Real Madrid – Liverpool | 2017–18 UEFA Champions League | 26 May 2018 | ||
Denis Cheryshev | Russia – Croatia | 2018 FIFA World Cup | 7 July 2018 | ||
Lazaros Christodoulopoulos | AEK Athens – Olympiacos | 2017–18 Superleague Greece | 24 September 2017 | ||
Giorgian De Arrascaeta | Cruzeiro – América Mineiro | 2018 Campeonato Mineiro | 4 February 2018 | ||
Riley McGree | Newcastle Jets – Melbourne City | 2017–18 A-League | |||
Lionel Messi | Nigeria – Argentina | 2018 FIFA World Cup | 26 June 2018 | ||
Benjamin Pavard | France – Argentina | 2018 FIFA World Cup | 30 June 2018 | ||
Ricardo Quaresma | Iran – Portugal | 2018 FIFA World Cup | 25 June 2018 | ||
Cristiano Ronaldo | Juventus – Real Madrid | 2017–18 UEFA Champions League | 3 April 2018 | ||
Mohamed Salah | Liverpool – Everton | 2017–18 Premier League | 10 December 2017 |
Tuzo Ya Mashabiki Bora.
MAshabiki | Mchezo | Mashindano | Tarehe | ||
Sebastián Carrera | Coquimbo Unido – Deportes Puerto Montt | 2017 Primera B de Chile | 22 October 2017 | ||
Mashabiki wa Japan na Senegal | 2018 FIFA World Cup | June 2018 | |||
Mashabiki wa Peru | 2018 FIFA World Cup | June 2018 |
Hafla ya kutangaza washindi wa tuzo za FIFA kwa mwaka 2018 imepangwa kufanyika septemba 24 katika ukumbi wa Royal Festival jijini London, England.