Klabu ya Barcelona inaweza kufungiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kushtakiwa kwa madai ya kuwahonga waamuzi.
Machi mwaka huu, Gazeti la SunSport iliripoti miamba hiyo inaweza kuondolewa katika mashindano hayo makubwa endapo itapatikana na hatia.
Chombo cha habari kutoka Hispania El Debate kinaripoti Jaji, Joaquin Aguirre ameishutumu Barcelona baada ya kutoa rushwa.
Hii inahusiana na malipo ya Pauni 6 milioni aliyohongwa Jose Maria Enruquez Negreira makamu wa rais wa zamani wa Kamati ya Ufundi ya Waamuzi.
Marais wa zamani wa FC Barcelona Maria Bartomeu na Sandro Rosell wote wamefunguliwa mashtaka, pamoja na mtoto wa Negreira, Javier Enriquez Romero.
Mabingwa hao watetzi wa La Liga wanashutumiwa kwa kukiuka sheria inayopiga marufuku maafisa kupokea hongo kwa utendaji.
Mashtaka hayo yanadai kuwa Negreira (makamu wa zamani kamati ya kiufundi ya waamuzi) alipewa pesa kupitia Kampuni ya Shell iliyoanzishwa na mkurugenzi wa zamani wa Barcelona Josep Contreras.
Refa wa zamani Alberto Gimenez pia amemshutumu Negreira kwa kumwita ‘kuku’ katika mkutano wa siri wa kupanga matokeo.
Aliiambia Radio Marca: “Negreira alinishinikiza. Alinikutanisha na waamuzi wengine na kuniambia: Wewe kuku, kuwa mwangalifu na unachosema. Nadhani umenielewa. Kuwa muangalifu.”
Rais wa LaLiga Javier Tebas alimuomba rais wa sasa wa Barcelona Joan Laporta kutoa ufafanuzi wa suala hilo haraka iwezekanvyo.