Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wanafikiria kutuma ofa nyingine ya Pauni 80 milioni kwa Tottenham ili kumnasa mshambuliaji, Harry Kane ikiwa ni siku kadhaa tangu ofa yake ya kwanza ya Pauni 60.2 milioni ilipokataliwa.

Kane ambaye mkataba wake unamalizika mwakani anauzwa kwa zaidi ya Pauni 100 milioni na Spurs imeshikilia msimamo wa kwamba bei yake haitashuka.

Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Ujerumani zinadai FC Bayern Munich imeshafanya makubaliano binafsi na Kane na kinachotazamiwa kwa sasa ni makubaliano baina ya timu hizo mbili.

Munich imekuwa ikimuangalia Kane kama sehemu ya maboresho ya eneo lao la ushambuliaji linaloonekana kukosa mtu sahihi tangu kuondoka kwa Roberto Lewandowski.

Timu kadhaa kutoka England zimeonyesha nia ya kumtaka Kane lakini staa huyu anaonekana kuitamani zaidi Munich kwa sababu ya uhakika wa asilimia nyingi za kuchukua mataji.

Wizara, Taasisi zatakiwa kupunguza matumizi ya fedha
Umuhimu wa urithi Kidijitali watumiaji simu za mkononi