Wafanyabiashara ambao wanaomba Leseni za kufungua Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kwa Benki Kuu ya Tanzania – BoT, wametakiwa kutotumia madalali.

Ushauri huo, umetolewa na Maofisa wa BoT waliofika Mkoani Kagera na kutoa ufafanuzi juu ya kanuni mpya za mwaka 2023 zilizofanyiwa marekebesho kutoka kanuni za mwaka 2019 kuhusu kufungua maduka na matawi ya kubadilishia fedha za kigeni.

Mkuu wa kitengo cha uchunguzi BoT, Amri Mbalilaki amesema kanuni za mwaka 2023 za kumiliki duka la kubadilisha fedha za kigeni zimepunguza vikwazo kwa Watanzania wazawa kupata leseni za umiliki, ukilinganisha na miaka ya nyuma hivyo hakuna sababu kutumia dalali.

Amesema, kwa miaka iliyopita mfanyabiashara aliyetakiwa kufungua duka la kubadilisha fedha za kigeni alipaswa kuwa na mtaji wa Sh bilioni moja na kuendelea lakini kwa sasa serikali imeondoa kikwazo icho kwani mfanyabiashara ambaye anamtaji wa Sh milioni 500 anaweza kumiliki duka la kubadilisha fedha za Kigeni.

Kwa upande wake Meneja msaidizi katika Kitengo cha usimamizi wa fedha kutoka Bank Kuu, Omary Msuya alisema ni lazima kuhakikisha fedha zinadhibitiwa na zinajulikana kiasi chake kuliko kuziacha zikabadilishwa kiholela katika mitaa na kutoa mwanya kwa matapeli.

Metacha avuruga mambo Young Africans
Duglas Luiz ainyima usingizi Arsenal