Rapa Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q, ameeleza kuwa heshima kubwa aliyopewa kushiriki katika msimu wa Coke Studio jijini Nairobi kwake ni upendeleo mkubwa.

Akifanya mahojiano maalum na tovuti ya Coke Studio, Fid Q ameshukuru kwa kupewa nafasi ya kuonesa umma kile ambacho alipaswa kuwaonesha.

“Kwakweli imenifanya nijione kama nimependelewa na nimebarikiwa mno. Ninashukuru kuwa nimeweza kuwakilisha kitengo cha Hip- Hop vizuri na nimeweza kuwasilisha kile ambacho watu walikuwa wakitarajia,” alisema Fid Q.

Rapa huyo alieleza kuwa muziki wa ‘live’ unaofanywa kupitia msimu huo unamfanya aone kuwa hivyo ndivyo msanii anatakiwa kufanya muziki wake. Alisema kuwa watu wengi walioshuhudia performance zake na Maurice Kirya kupitia msimu huo, wamekuwa wakimpongeza na kumtaka afanye kazi kwa kiwango katika muziki wake.

“Cha msingi wanachokifanya Coke Studio ni kutabiri mustakabali wako wewe kama msanii kwamba hivyo ndivyo unavyotakiwa kufanya,” alisema.

 

Magufuli Awaita Ukawa ‘Watoto’, Spika Awapa Onyo Kali, Asema Atakuwa ‘Mbabe’
Wabunge Wa Ukawa Watolewa Nje ya Bunge