Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Pablo Franco Martin amesema yupo tayari kwa mpambano wa kesho Ijumaa (Novemba 19) wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting.
Mchezo huo ambao umepangwa kuanza majira ya saa kumi jioni Uwanja wa CCM Kirumba , utashuhudia Simba SC ikicheza ugenini kwa mara ya tatu, tangu kuanza kwa msimu huu 2021/22.
Kocha huyo kutoka nchini Hispania amezungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza leo Jumatano (Novemba 18) na kusema: “Tunategemea mchezo mgumu lakini tuko tayari kwa mchezo wa kesho. Tunajua ni mchezo muhimu na tutapambana ili tupate alama tatu.”
Simba SC inakwenda kwenye mchezo wa kesho ikiwa na alama 11 zinazoiweka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Ruvu Shooting ikiwa na alama 6 zinazoiweka nafasi ya 10.
Simba SC ilishinda mchezo wake uliopita dhidi ya Namungo FC kwa bao 1-0, huku Ruvu Shooting ikipoteza mbele ya Young Africans kwa mabao 3-1.