Frank Lampard amedai kuwa kurudi kwake Chelsea kwa mara nyingine ni kuheshimiwa na mmiliki wa klabu, Todd Boehly, ingawa hana uhakika kama James Corden rafiki wa karibu na Boehly alishinikiza yeye kupewa kazi hiyo.

Gwiji huyo wa Blues ameajiriwa kama kocha wa muda hadi mwisho wa msimu kufuatia Graham Potter kutimuliwa.

Boehly anatafuta kocha mwingine wa kudumu na wakati akifanya hivyo, ripoti zinadai mchekeshaji huyo wa Kiingereza ambaye ni rafiki wa karibu sana na Boehly alipendekeza ampe Lampard jukumu hilo hadi mwishoni mwa msimu huu.

Lampard, 44, aliteuliwa siku nne baada ya Potter kutimuliwa ikiwa ni msimu wa kwanza wa Chelsea chini ya umiliki wa Mmarekani huyo ukiendelea.

Lampard alisema: “Ninapoangalia mafanikio ya Todd Boehly na wamiliki wa Klabu ya Soka ya Chelsea nadhani unapaswa kuheshimu mafanikio hayo na kuheshimu wazo kwamba watafanya maamuzi kwa kuzingatia zaidi ya mazungumzo na mtu mmoja.”

Lampard hadi sasa amesimamia mechi mbili Chalsea na zote amepigwa, ya kwanza ilikuwa ya Premier dhidi ya Wolves na juzi UEFA ambapo walipigwa 2-0 na Real Madrid.

Majaliwa ataka Wazazi waimarishe uhusiano na watoto
Baada ya kutua Bungeni, taarifa ya CAG yaanza kufanyiwa kazi