Njia bora zaidi ya kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali ni kuhakikisha usafi wa mikono ili kuzuia vijidudu vya magonjwa, mtu anashauriwa kunawa mikono kwa maji na sabuni hata ikiwa mikono inaonekana safi kwani inawezaka kuwa na vijidudu au mayai ya minyoo.
Vidudu hivyo vinaweza kusababisha kuugua kama vitaingia mwilini kwa njia zozote zile ikiwa ni pamoja na chakula chako.
Unashauriwa kunawa mikono mara kwa mara ili kuzuia vidudu vyenye maradhi kuingia mwilini.
Unashauriwa kunawa mikono yako kila baada ya kupiga chafya au kukohoa, baada ya kwenda msalani/kujisaidia au kumtawaza mtoto, kabla ya kuandaa chakula au kula, baada ya kukamata wanyama wa aina yoyote.
Utaratibu unaofaa wakati wa kunawa mikono unafaa kuzingatiwa kila mara kwani unaweza kuhisi umenawa vizuri kumbe bado kuna vidudu hatari vilivyojificha.
Utaratibu au hatua za kunawa mikono:
1. Mimina maji kwenye mikono yako, Mikono yenye sabuni ikisuguana na mikono yenye sabuni ikisuguana
2. Tumia sabuni na usugue mikono pamoja. Kumbuka kuwa, msuguano huo ndio utakaondoa vijidudu hivyo. Pia wakati unapofanya hivyo, hakikisha unasugua katikati ya vidole na kuzunguka kucha za vidole.
3. Kisha mimina maji safi kwenye mikono yako na kuisuuza vizuri.
4. Ukimaliza, ikaushe mikono kwa kitambaa safi. Katika maeneo ambako labda sabuni haipatikani rahisi, ni bora kutumia mchanga au majivu kuondoa vijidudu hatari. Nawa mikono kila baada ya muda mfupi.