Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka watumishi wa umma kuanza kujipanga na maisha kabla ya kustaafu ili kuweza kuondoa hofu ambayo imekuwa ikiwakabili wakati muda wao wa kustaafu unapowadia.
Ameyasema hayo wakati wa akifunga mkutano wa mfuko wa mafao ya kustaafu GEPF uliofanyika jijini Arusha, amesema kuwa kwa sasa wastaafu wanapata magonjwa mbalimbali hasa ya moyo kwa sababu hawajajiandaa kubuni miradi itakayo waingizia kipato.
Amesema kuwa maandalizi ni mhimu sana kwa wafanyakazi hata kama bado hawajafikia muda wa kustaafu kwani kustaafu sio ajali bali ni utaratibu uliowekwa kwaajili ya kutoa nafasi kwa wengine.
“Wastaafu wengi wanakufa pindi wanapo staafu, sio sawa hata kidogo lazima kila mtu ajiandae na abuni njia mojawapo ya kujiingizia kipato kwani hata kama ukijiajili mwenyewe lazima utapata kipato,“ amesema Gambo.
Hata hivyo, Gambo amewataka wakuu wa mifuko ya hifadhi hapa nchini kuhakikisha wanatoa elimu ya kujiandaa kustaafu kwa wafanyakazi wake kwani asilimia kubwa inaonyesha hawana elimu hiyo