Rais wa ufaransa Emmanuel Macron na Vladimir Putin wa Urusi wameseme kuwa kipaumbele chao katika ushirikiano wa nchi zao kitakuwa ni kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Syria ili kuondokana na vitisho vya kigaidi.

Aidha, katika mkutano huo uliofanyika Ikulu ya Versailles karibu na mji wa Paris, marais hao wamekubaliana kuwepo kwa mazungumzo ya Ujerumani kuhusu mzozo unaoendelea nchini Ukraine ambapo Urusi inatuhumiwa kuchochea na kutaka kuligawa taifa hilo.

Hata hivyo, Putin amekanusha taarifa ambazo zimezagaa kuwa Urusi ilijiingiza katika uchaguzi mkuu wa Ufaransa uliomalizika hivi karibuni na kusema kuwa kukutana kwake na mpinzani wa Macron, Marine Le Pen wakati wa kampeni hakukuwa na uhusiano wowote na matokeo ya uchaguzi.

Video: Mangu afunguka, Mchanga wa dhahabu waacha vumbi bungeni
Gambo atoa neno kwa watumishi wa umma