Vijana wameshauriwa kutokimbia changamoto bali kuzikabili na kuwa chachu ya kupambana zaidi ili aweze kufikia ndoto zake.
Ushauri huo umetolewa na Mshereheshaji mahiri nchini na Afrika mashariki Godfrey Rugarabamu maarufu kama Mc Gara B, wakati akizungumza na Dar24 Media.
Amesema “penye nia pana njia na mwisho wa siku kijana au mtuu yeyote kama yupo hai na ananguvu haijalishi anapitia mapito yapi yasiwe changamoto kwakwe bali chahchu yay eye kupambana zaidi.”
“tusiwe wagumu kujifunza kitu kipya kwenye kukabiliana na hizi changamoto za maisha kama kuna nafasi ambayo umeipata nenda pale itumie na usichukulie poa ona hii ni fursa uone kama umepewa nafasi nyingine,” amesema Gara B
Ameongeza kuwa, “kwamfano darasa ambalo nilikuwa nafundisha nililikuwa linafaulu na kama walimu wanapewa zawadi za kuwamotivate mimi nilikuwa nakula sana zawadi sababu nafaulisha.”
“Kwahiyo nafasi yoyote ambayo unaipata uitumie usiichukulie poa iwe kama umepewa kwa mara ya pili iwe kama ukitoka hapa ndo umekufa kwahiyo usiogope kujifunza nenda kaifanya halafu pambania jambo lako,” amesema Gara B.