Nyota wa muziki wa Afro beat kutoka nchini Nigeria, Guchi amerejea kwa kasi kwenye vichwa mbali mbali vya habari baada ya kuachia nyimbo mbili mfululizo
zenye kuijenga taswira ya kumsogeza kwenye orodha ya wasanii mahiri wa kike wenye kufanya vyema zaidi barani Afrika.

Nyimbo hizo ambazo ni ‘ALL OVER YOU’ na MON BEBE, zimetayarishwa na Shugavybz pamoja na Kaelbeatz wote kutokea nchini Nigeria.

Upekee kwenye maudhui ya nyimbo hizo zinazozungumzia mapenzi unatokana na hadithi za mapenzi zenye kusisimua akizungumzia mahusiano yalivyo mlewesha na kiasi cha kuwa tayari kupambana na kushikamana hadi kufa kwenye mahusniano hayo.

Wimbo Mon Bebe iliyotayarishwa na Kaelbeatz,Purple girl ameuelezea furaha na kila kizuri anacokipata kwa mpenzi wake ikiwamo kupata vipele vidogo vya mapenzi kila anapomuona.

awamu hii kwenye nyimbo zote, Guchi amekuwa akisimulia mfululizo wa hadithi ya mapenzi iliyojawa visa vya kusisimua.

Swali la wengi ni ipi sababu ya nyota huyo kurejea na nyimbo mbili kwa mkupuo mmoja?, huku kundi la baadhi ya mashabiki wakikihusisha kitendo hicho na kujidhatiti kiushindani sokoni dhidi ya wasanii wenzie hasa wakike wenye kufanya vizuri kwa sasa kwenye tasnia ya musiki barani Afrika.

Ikumbukwe kabya ya mradi huu Guchi aliachia extended playlist yake Purple Diary iliyofanikiwa kufanya vizuri mapema mwaka 2022.

Wizara yapewa kibali kuajiri Watumishi sekta ya Afya
Taasisi zinazokopesha wachimbaji wadogo kufuatiliwa