Serikali ya Afghanistan imeituhumu Pakistan kwa kuwaunga mkono wanamgambo ambao wamefanya shambulio lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 95 na wengine 158 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu la kujitoa mhanga mjini Kabul.

Imesema kuwa shambulio hilo la jana Jumamosi, lililotekelezwa na kundi moja la wapiganaji la Haqqani, lenye uhusiano mkubwa na lile la Taliban, linaungwa mkono na Pakistan.

Aidha, Utawala wa Afghanistan, umesema kuwa shambulio hilo limekuwa ni kubwa zaidi ikilinganishwa na mashambulio yaliyopita, kitu ambacho hakiwezi kuvumiliwa.

Pakistan imekanusha taarifa hizo za Afghanista za kuyaunga mkono makundi ya wanamgambo yenye nia ya kuhujumu utawala wa Afghanistan.

Hata hivyo, wanamgambo hao wametumia gari la wagojwa kufanya shambulio hilo katika kituo cha usalama mara baada ya kusimamishwa na askari kwa ajili ya ukaguzi.

Video: Lowassa atoboa siri, Wamekwisha
Lowassa awaziba midomo Chadema