Ukraine imeituhumu Urusi kuwa inaihujumu Ulaya kwa kusitisha usambazaji wa gesi nchini Poland na Bulgaria wakati mzozo wa nchi hizo mbili ukiendelea, Hata hivyo Nchi hizo zimekataa kulipia gesi katika sarafu ya Kirusi ya ruble
Poland, ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO na mkosoaji mkubwa wa Urusi ni miongoni mwa nchi za Ulaya zinazotafuta vikwazo vikali zaidi dhidi ya Urusi kwa uvamizi wake. Huku mwanachama mwenza wa NATO Bulgaria ikitegemea pakubwa gesi ya Urusi.
Kampuni ya gesi ya Poland inayomilikiwa na serikali PGNiG imesema usambazaji wa gesi kutoka kampuni kubwa ya nishati ya Gazprom kupitia Ukraine na Belarus utasitishwa leo asubuhi, lakini Warsaw imesema wateja wake hawapaswi kuwa na wasiwasi kwa sababu hifadhi yake ya gesi ni asilimia 76.
Rais wa Urusi Vladmir Putin amezitaka nchi anazoziita zisizo za kirafiki kulipia bidhaa za gesi katika sarafu ya rouble, hatua ambayo ni wanunuzi wachache tu ndio wameitekeleza mpaka sasa.
Andriy Yermak, mkuu wa utumishi katika ofisi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Urusi inajaribu kuuvunja umoja wa washirika wa Ukriane kwa kutumia raslimali za nishati kama silaha.