Waziri wa Nishati wa Kenya, Davis Chirchir ametetea kupanda kwa bei za mafuta akisema hali hiyo imesababishwa na hatua iliyochukuliwa na Taifa la Saudi Arabia na Russia, kupunguza uzalishaji wa bidhaa hiyo na kusababisha bei ya mafuta ghafi kupanda kwenye soko la Dunia.
Hali kufikia Septemba 15, 2023 Bei ya mafuta nchini Kenya imefikia kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa baada ya mamlaka ya Nishati kurekebisha bei kwenye vituo vya mafuta, hali liyopelekea kuongezeka kwa ugumu wa maisha kwa wakazi na jamii wa Wakenya.
Hata hivyo, Wakenya pia wamekuwa wakikabiliwa na gharama kubwa ya maisha kutokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa za chakula, msururu wa kodi mpya zilizoainishwa na Serikali na kushuka kwa thamani ya shillingi ya Taifa hilo.
Bei mpya za hadi Oktoba 14, 2023 zinaonesha kuwa bei ya lita moja ya Petroli katika Mji Mkuu wa Nairobi imeongezeka kwa shilingi 17 na kufilia shilingi 211.64, huku bei ya Mafuta ya Dizeli ikipanda hadi shilingi 200.99 na mafuta ya Taa yakiwa shilingi 202.61.