Ili demokrasia iwe na maana kwa maisha ya wananchi ni lazima ilete matokea katika huduma muhimu za jamii na kuboresha maisha wananchi, ikiwemo kupatikana kwa njia thabiti iliyothibitishwa kuwaunganisha wananchi.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan hii leo Julai 17, 2023 jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa wadau wa Demokrasia Afrika, ambao utahusisha viongozi wakuu wastaafu wa Afrika.

Amesema, “Serikali kushindwa kutoa huduma kwa wananchi ndio sababu ya kuanzisha kwa mifumo ya kuwasilisha mahitaji ya wananchi kama uwepo wa wanaharakati, maandamano kushinikiza upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi na hapa ndipo uhuru wa kujumuika na kutoa maoni unapotumika tofauti.”

Aidha, Dkt. Samia pia amesema ameanzisha R nne ambazo ni maridhiano (Reconciliation), mabadiliko (Reforms), ustahimilivu (Resilience) na kujenga upya (Rebuilding) lengo kuu lilikuwa kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahimilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma amesema utawala wa sheria umeleta umoja na uongozi bora kwa nchi za Afrikana kwamba yapo mambo yanaendelea katika mataifa ya Nigeria, Burkinafaso na Congo ambayo yanaacha maswali kuliko majibu.

Morrison, Bangala wanawindwa Singida FG
Man Utd yajitafuta usajili wa mshambuliaji