Takriban watu watano wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa sita kuporomoka (Septemba 26) katika eneo la Kiambu, pembeni kidogo mwa mwa jiji la Nairobi nchini Kenya.
Idara ya Zimamoto na Majanga ya Kaunti ya Kiambu, Polisi na Vikosi vya Ulinzi vya Kenya, pamoja na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya imesema watu kadhaa walitolewa kutoka kwa vifusi wakiwa hai wakati wa alasiri, wengi walihofiwa kuwa bado wamenaswa katika eneo hili..
Gavana wa kaunti ya Kiambu, Kimani Wamatangi amesema ujenzi wa jumba hilo la orofa nyingi haukuwa halali na chanzo kilichosababisha jengo hilo kuporomoka hakijabainika lakini Juhudi za uokoaji zinaendelea na wafanyakazi wa dharura wamefanikiwa kuwaokowa watu kadhaa akiwemo mtoto kutoka kwenye vifusi.
Amesema, “Pia nimepata uthibitisho kutoka kwa CEC yangu (Kamati ya Utendaji ya Kata), inayosimamia kuwa jengo hili halikuidhinishwa, kwamba mtu huyu alijenga bila kibali, alikuja na kuomba kibali, na aliambiwa kuzingatia masharti machache. , alitoweka aliendelea kujenga na ni leo tu tumemuona.”
Hata hivyo, mashuhuda wanasema jengo hilo pia liliangukia nyumba za mabati na zingine zilizokuwa pembeni na haijulikani ni watu wangapi bado wako chini ya vifusi, huku wanajeshi, wafanyikazi kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na wafanyikazi wa Huduma ya Vijana ya Kitaifa, pamoja na wajitolea wa ndani wameshiriki zoezi la ukoaji.
Ajali za majengo kuporomoka, zimekuwa zikitukia maeneo mengi barai Afrika, ikiwemo nchi ya Kenya ambayo inalaumiwa kwa kuwa na uangalizi dhaifu, ufisadi na vifaa duni vya ujenzi, na inaarifiwa kuwa majeruhi walisafirishwa hospitali zilizo karibu huku Gavana huyo akitembelea baadhi ya waliolazwa katika Hospitali ya Kiambu ya Level V.