Viungo Mzamiru Yassin (Tanzania), Clatous Chotta Chama (Zambia) na Mshambuliaji Moses Phiri (Zambia) wametajwa kuwania tuzo ya mchezo bora wa Simba SC mwezi Septemba 2022.

Simba SC imewataja watatu hao kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii mapema leo asubuhi (Septemba 27), kufuatia uwezo mkubwa waliouonyesha katika Michezo ya Simba SC.

Taarifa iliyowekwa kwenye Mitandao ya Kijamii ya Simba SC imendikwa: “Hawa hapa ndio wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) mwezi Septemba ni; Moses Phiri, Clatous Chama na Mzamiru Yassin.”

“Tembelea tovuti yetu ya simbasc.co.tz ili kupiga kura.”

Taarifa hiyo inatoa nafasi kwa Mashabiki wa Simba SC kuanza mchakato wa kupiga kura, ili kumpata mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora kwa mwezi Septemba.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Kiungo Chatous Chotta Chama kuingia katika kinyang’anyiro hicho, baada ya mwezi uliopita kutajwa kwenye orodha iliyokua na Mshambuliaji Osman Sakho (Senegal) na Kiungo Sadio Kanoute (Mali).

Kiungo Clatous Chotta Chama alitangazwa kuwa Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Simba SC, akipata kura nyingi zaidi ya Osman Sakho na Sadio Kanoute.

Al Hilal yamnyima usingizi Fiston Mayele
Ghorofa jingine laporomoka, watano wafariki