Usiku wa kuamkia leo nchini Marekani kumepigwa pambano la masumbwi kati ya Canelo Alvarez na Gennady Golvkin ambalo wafuatiliaji wengi wa masumbwi walikuwa wakulisubiri kwa hamu, pambano hilo limemalizika kwa maamuzi ya kutatanisha baada ya majaji wa pambano hilo kuamua kuwa sare.
Kila shabiki aliona bondia wake anashinda kutokana na makonde yalivyorushwa katika pambano hilo lakini majaji wakuwatoa maamuzi tofauti; Adalaide Byrds akimpa Alvarez pointi 118-110, Dave Merrotti akampa Golvkin 115-113, huku Don Trella akiamua sare ya kwa kuwapa 114 kwa 114.
Katika panbano hilo Mashabiki 22,358 waliojitokeza walitaraji kuona ‘knock out’ ikitokea kutokana na ngumi zilivyokuwa zinapigwa lakini mwisho wa siku waliona Golovkin akibaki na mikanda yake ya WBC,WBF na WBO katika ngazi ya middleweight.
-
Dunia kushuhudia pambano la mwaka la masumbwi leo, Canelo Vs Triple G
-
Hodgson aanza kwa kipigo Crystal Palace
-
Bondia McGregor apeleka ubabewake kumbi za Starehe
Watu wengi waliotazama pambano kati ya Conor McGregor na Floyd Mayweather walikosoa sana pambano hilo, wengi wakidai yalikuwa maigizo na watu hawakuwa ‘serious’ kuhusu ngumi lakini pambano hili la Canelo Alvarez na Gennady Golvkin pia limeachwa maswali
Canelo Alvarez na Gennady Golvkin walivaana katika uwanja wa T Mobile mjini Las Vegas nchini Marekani katika pambano hilo lililomalizika kwa sare.