Wakimbizi wasiopungua 18 wameuliwa na jeshi DRC ambapo inasemekana kuwa idadi hiyo inaweza ikaongezeka kwakuwa mashambulizi dhidi ya wakimbizi hao yalikuwa makubwa.

Wanajeshi wa Congo wamewapiga risasi na kuwauwa wakimbizi hao kutoka nchi jirani ya Burundi kufuatia mapigano yaliyozuka katika eneo la Kamanyola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Hayo yamesemwa na maafisa wa eneo hilo katika Mkoa wa Kivu Kusini na kutoa idadi hiyo ya awali ambapo wametahadharisha kuwa inaweza ikaongezeka wakati wowote kulingana na ukubwa wa shambulizi hilo.

Aidha, Afisa mmoja kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, Josue Boji amesema kuwa wanajeshi walikuwa wakijaribu kuwatawanya wakimbizi hao kwa kufyatua risasi hewani lakini walizidiwa nguvu baada ya kundi kubwa la wakimbizi hao kulivamia gereza moja wakitaka warundi wanne wanaoshikiliwa katika gereza hilo waachiwe huru.

Hata hivyo, Warundi wengi walikimbilia DRC ili kuepuka vurugu zilizoikumba nchi yao mwaka 2015 baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kuamua kugombea tena nafasi ya urais kwa muhula wa tatu.

 

Nyumba yamtia matatani Zitto Kabwe
Golovkin na Canelo hakuna mbabe