Mkurugenzi wa Uwekezaji kampuni ya GSM Mhandisi Hersi Said amesema kwa kiasi kikubwa wameridhishwa na mapokezi ya mashabiki wa Young Africans katika ununuzi wa jezi za klabu yao.

Hersi amesema muamko huo umewapa hamasa ya kuendelea kufanya kazi na Young Africans huku akiwaahidi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kukaa mkao wa kula kwa mapokezi ya jezi mpya, kwa ajili ya msimu ujao ambazo zitakuwa bora zaidi kuliko za msimu huu.

“Tulitoa matoleo mawili ya jezi yaani Grade A na Grade B. Pamoja na uwepo wa changamoto ya jezi feki, muamko wa ununuzi wa jezi halisi umekuwa mkubwa sana.”

“Wanayanga wameonyesha kupenda vitu bora kwani hata ukiangalia takwimu za mauzo, zile za Grade A ambao tunaziuza Tsh 35,000/- ndizo zinazonunuliwa zaidi kuliko za Grade B ambazo awali tulikuwa tukiziuza Tsh 25,000/- na sasa tunaziuza Tsh 20,000/- pamoja na nakala ya jarida la klabu ya Young Africans.” Alisema Mhandisi Hersi Said

Aidha Hersi amesema kuelekea msimu ujao wamejipanga kunufaika na mauzo ya jezi za wachezaji wapya ambao watawasajili

“Tunawaambia Wanayanga wakae tayari, kuna usajili mkubwa sana ambao tutaufanya mwaka huu”

Young Africans imehusishwa na taarifa za usajili wa wachezjai kadhaa kuelekea msimu ujao wa ligi, ambapo wamedhamiria kurejeshwa ubingwa wa Tanzania bara kutoka kwa watani ao Wekundu Wa Msimbazi Simba.

Hakuna visa vipya vya corona – Rwanda
Marekani yaja na mkakati wa kufungua Uchumi