Rais Donald Trump wa Marekani amesema Kikosi Kazi cha Ikulu kinachosimamia janga la COVID-19 kinatarajiwa kuvunjwa na mkakati uliopo hivi sasa ni kufungua uchumi wa nchi hiyo.

Akitembelea kiwanda cha kutengeneza barakoa (mask) kilichopo Arizona amesema ni kweli kuna watu wamethirika vibaya lakini inapaswa kufungua taifa hilo mapema.

Ameongeza kuwa Kikosi hicho kimefanya kazi nzuri hadi sasa lakini Marekani haiwezi ikaendelea kufungwa kwa miaka mitano ijayo, hivyo kinachoangaliwa kwa wakati huu ni usalama na kufungua nchi.

Kwa mujibu wa CNN. Kikosi hicho kiliundwa Januari mwaka huu na Makamu wa Rais, Mike Pence alitajwa kuwa Mwenyekiti.

Mtoto wa miezi 6 aambukizwa corona, visa vyaongezeka Kenya

Rais Trump amesema wataalamu wawili wa ngazi ya juu, Anthony Fauci na Deborah Birx watabaki kama washauri.

Mpaka hivi sasa Marekani imeathirika zaidi na mlipuko wa virusi vya Corona kuliko nchi yoyote duniani, huku ikiwa na na takribani visa 1,312,960 na vifo 74,429 huku waliopona wakiwa 184,220.

Corona: NIMR-Tanzania yatengeneza dawa asili kuwasaidia wagonjwa

GSM wapongeza na kuahidi makubwa Young Africans
Corona: Serikali yaendelea kushughulikia changamoto zinazojitokeza mipakani